Zanzibar Quality bakery

Zanzibar Quality bakery Zanzibar Quality bakery ni wahusika wa kupika Vyakula mbalimbali vikiwemo Biriani,Pilau,Keki,Vileja,Mikate,Sandwich na vyakula vyenginevyo kwa bei nafuu

Ili kupata taarifa za mapishi,habari na mafunzo ya kupika subscribe channel yetu YouTube Zanzibar Online Media utapata taarifa kila zinapotoka

Mapishi ya Sambusa Za NyamaMahitaji½ kilo Nyama ya iliyosagwakijiko 1 kikubwa cha chakula cha Pilipili manga▪︎Vitunguu m...
30/05/2022

Mapishi ya Sambusa Za Nyama

Mahitaji

½ kilo Nyama ya iliyosagwa

kijiko 1 kikubwa cha chakula cha Pilipili manga

▪︎Vitunguu maji vinne

Kijiko kimoja cha chakula cha kitunguu Thomu na tangawizi iliyosagwa

Mafuta ya kupikia Kiasi

Vijiko vinne unga ngano au ute wa yai kwa kufungia sambusa

Kaki za sambusa (unaweza kununua zilizokuwa tayari zimeshakatwa kwa ajili ya sambusa au k**a utanunua zile sheet pana utazikata kwa inchi 4 upana wa ruler yaani upate mistari 3

Maelekezo

Kausha nyama ya kusaga kwa kiyunguu swaumu (thomu) na tangawizi pamoja na chumvi mpaka ikauke vizuri Iwache ipoe.

Kata kata majani ya kotmiri weka upande Kata kata upate vipande vidogo vidogo(chop) vya vitunguu maji.

Zikate pili pili zako slice za mviringo vidogo vidogo.

Wakati ukimaliza matayarisho haya na nyama yako itakuwa ishapoa kabisa hapo ndio utachanganya,bizari nzima pamoja na pilipili manga pamoja na vitu vyote ulivyokwisha vitayarisha

Koroga unga ndani ya kibakuli au ute wa yai

Weka kaki kwa mfungo wa triangle yaani pembe tatu k**a kofia na

weka mchanganyiko wa nyama yako kiasi na uanze kuzifunga sambusa zako na ukifika mwisho hapo ndipo upake unga wako kwa ajili ya kuifunga isifunguke wakati wa kuchoma, pendelea kutumia kaki 2 kwa kila sambusa moja.

Kuchoma kwake ikiwa unazifanya na kuzichovya hapo hapo mafuta lazima yawe baridi (ninakusudia uweke mafuta na uzitie sambusa kabla hayajapata moto).

Na ikiwa uliziweka kwenye friji zikaganda basi unatakiwa uzichome kwa mafuta ya moto

Like, Comment uliza ikiwa hujaelewa kisha share na wenzako

JINSI YA KUTENGENEZA JUICE YA EMBE Mahitaji1. Maembe2.sukari3. TangawiziHATUA1. Chemsha maji ya kutosha mfano lita 2 had...
30/09/2021

JINSI YA KUTENGENEZA JUICE YA EMBE
Mahitaji
1. Maembe
2.sukari
3. Tangawizi

HATUA
1. Chemsha maji ya kutosha mfano lita 2 hadi 5 kulingana na wingi wa matunda

2.chukua matunda yako na uyaoshe vizuri kwa kutumia maji ya vuguvugu yaliyowekwa chumvi kiasi ili kuua vijidudu

3. Menya matunda yako taratiibu bila kujikata vidole

4.katakata matunda katika vipande vidogo vidogo ili kuiwezesha blender yako kusaga matunda kwa urahisi.

5.chukua matunda na tangawizi kidogo kisha weka katika brenda na anza kusaga.

Unaweza kuongeza maji yaliyochemshwa wakati wa kusaga ili kupata mchanganyiko wa wastani usio mzito sana.

6. Chukua maji yaliyochemshwa changanya na rojo la matunda kwa kiasi kulingana na wingi wa matunda kisha koroga.

7. Chukua chujio safi na chuja mchanganyiko wako huo. 

8. Chukua sukari na uitie katika mchanganyiko wako. Kisha koroga hadi sukari yote iyeyuke.

9. Chukua chombo safi maalum cha kuwekea juice na anza kuitia juice katika vyombo hivyo mfano Chupa za plastiki

10. Weka juice yako katika friji. Unaweza kunywa juice yako.

Good morning  fans 🌅🌅🌅
11/08/2021

Good morning fans 🌅🌅🌅

Dates biscuits
26/04/2021

Dates biscuits

Cake doughnuts
26/04/2021

Cake doughnuts

Vileja vya Custad
26/04/2021

Vileja vya Custad

Pumzika kwa amani baba
18/03/2021

Pumzika kwa amani baba

JINSI YA KUPIKA BIRYANI YA KUKU MAHITAJIVipande vya kuku kilo 1Mchele wa basmati gramu 500 (unaweza kutumia mchele unaop...
12/03/2021

JINSI YA KUPIKA BIRYANI YA KUKU

MAHITAJI
Vipande vya kuku kilo 1
Mchele wa basmati gramu 500 (unaweza kutumia mchele unaopenda)
Kitunguu maji nusu kilo
Nyanya zilokatwa 5
Vitunguu saumu punje 5
Pilipili za kijani 4
Mafuta ya kula vijiko vya chakula 4
Mdalasini vijiti 4
Hiliki 3-4
Tangawizi iliopondwa vijiko vya chakula 2
Majani ya nanaa yaliyokatwa kiganja 1
Binzari nyembamba kijiko cha chai 1
Chumvi kijiko cha chai 1
Manjano kijiko cha chai ½
Zaafarani kijiko cha chai ½ (si lazima)
Kotmiri iliyokatwa kikombe ¼

Matayarisho

Loweka mchele wa basmati kwenye maji na uweke pembeni kwa dakika 15 hadi 30 (k**a hutumii mchele wa basmati basi utaangalia mwenyewe mchele unaotumia)

Maelekezo

Weka mafuta kwenye sufuria, yakipata moto kaanga kitunguu maji hadi view na rangi ya kahawia.
Twanga kwa pamoja binzari nyembamba, kitunguu swaumu, tangawizi, nusu ya pilipili na vijiti viwili vya mdalasini, kisha weka kwenye vitunguu ukaange pamoja kwa dakika tatu.
Tia nyanya na pika kwa dakika tano
Tia vipande vya kuku koroga, acha iwive kiasi cha dakika 10 hadi 15 na ikaukie
Weka pilipili zilobaki kotmiri na masala ya kuku. Pika rosti liwe zito.
Acha rosti na weka pembeni.
Chemsha maji kwa hiliki na mdalasini na chumvi kisha weka mchele lakini usiwive kabisa kwa dakika tano baada ya hapo mwaga maji.
Panga wali na masala.
Kwanza chemsha maji ½ kikombe katika sufuria utakayopikia biryani. Maji yakishachemka anza kuweka wali kisha rosti na malizia na wali. K**a una tumia zaafarani…
Zaafarani kawaida hurowekwa kwenye vijiko vyenye maziwa ya vugu vugu na kumwagilia kwa juu.
Weka moto mdogo kwa dakika 30. Baada ya hapo chakula chako kitakuwa tayari.

JINSI YA KUPIKA MEAT ROLL MAHITAJI√ Siagi - Kikombe 1√ Unga - Vikombe 2√ Maji - Kiasi√ Nyama ya kusaga - Kikombe 1√ Pili...
04/03/2021

JINSI YA KUPIKA MEAT ROLL

MAHITAJI

√ Siagi - Kikombe 1
√ Unga - Vikombe 2
√ Maji - Kiasi
√ Nyama ya kusaga - Kikombe 1
√ Pilipili manga ya unga - ½ kijiko cha chai
√ Kitunguu saumu(thomu) iliyosagwa - ½ kijiko cha chai
√ Tangawizi iliyosagwa - ½ kijiko cha chai
√ Chumvi - kiasi

NAMNA YA KUTAYARISHA

Changanya nyama, pilipili manga, thomu, tangawizi na chumvi ndani ya sufuria, ipike bila ya kutia mafuta wala maji huku unaikoroga koroga mpaka iwe kavu.Epua weka pembeni

Changanya unga na siagi mpaka uchanganyike vizuri.

Changanya na maji ili ushikane, lakini usiukande.

Kata madonge na usukume k**a unataka kufanya chapati, lakini usifanye mwembamba sana.

Kata vipande virefu virefu. (rectangular)
Weka nyama juu ya kila kipande, halafu kunja upande mmoja ufunike ile nyama, kisha kunja upande wa pili kufunika ile sehemu ya kwanza uliyoikunja.

Chukua uma choma choma juu yake ili kuweka nakshi, pia utadidimiza ile sehemu ya mwisho iliyokunjwa kwa kuzuwia isifunuke wakati wa kuchoma.
Fanya hivyo mpaka umalize zote.

Chukua tray na kupaka siagi na uzipange humo.Washa oven na uzichome (Bake) 350C mpaka zibadilike rangi zikiwa tayari kuliwa.

USISEME UTAJARIBU PIKA SASA

SHARE NA WENZAKO WAPIKE NA LIKE POST HII

WALI WA ASUMINIMAHITAJIMchele kilo 1Kuku mkubwa 1Vitunguu maji kilo 2Mayai 8mafuta lita 1Thomu gram 200Tangawizi mbichi ...
27/02/2021

WALI WA ASUMINI

MAHITAJI

Mchele kilo 1
Kuku mkubwa 1
Vitunguu maji kilo 2
Mayai 8
mafuta lita 1
Thomu gram 200
Tangawizi mbichi gram 50
Mdalasini gram 50
Hiliki gram 50
Bizari nzima kiasi
Mtindi pakti 1
Tungule kilo 1
Zabibu nyeusi kiasi

MATAYARISHO
1 Mkate kuku umwoshe umchemshe kwa maji na chumvi mpaka awive, kisha muepue.
2 Menya vitunguu uvioshe uvikate na uvigawe sehemu mbili. Sehemu moja uiweke, sehemu ya pili vikaange mpaka viwe vyekundu k**a vya biriani. Kisha vichuje uitoe mafuta yote, vitie katika sinia uvitandaze ili vipoe kwa kupata upepo.
3 Chukua mdalasini, hiliki na bizari utwange pamoja, kisha uchunge unga laini. Saga thomu na tangawizi mbichi. Saga tungule.

4 Teleka sufuria tia mafuta yaleyale iliyokaangiwa vitunguu halafu utie vile vitunguu vilivyobakia uvikaange. Vikianza kuiva tia viungo ulivyovitwanga na kuvisaga. (Bakisha vitunguu na viungo kidogo). Tia vipande vya kuku, mtindi na supu ya kuku iliyobakia katika sufuria. Acha ichemke nyama pamoja na vitu vyote mpaka libaki rojorojo.

5 Teleka maji, yakichemka tia chele. Ukiiva utoe uchuje yatoke maji yote.

6 Teleka tena sufuria utie mafuta kidogo utie na vile vitunguu ulivyovibakisha uvikaange. Tia mdalasini nzima, kaanga pamoja, tia na ule wali ukoroge koroge ili uchanganyike na viungo. Kisha ufunike upalie moto.

7 Chemsha mayai yote uyamenye.

8 Wali ukishakauka utaupakua, lakini lazima itabidi utumie kombe au sahani kubwa itakayoweza kuingia wali pamoja na vitu vyote. Kuupakua kwake kwanza utatia nusu ya wali katika hiyo sahani, baadae utatia masalo na nyama yote, na mayai, kisha utayafunika masalo kwa wali uliobakia.

Mwisho utachukua vile vitunguu ulivyovikaanga na ukavitandaza ili vipo, utavimwaga juu ya wali.Kwani ni kwa sababu ya hivi vitunguu ndio maana ukaitwa wali wa asumini. Ukipenda utapamba chembe za zabibu juu yake. ZABIBU HIZO Ziroweke kwanza ili zivimbe

CHAKULA KIKIIVA USISAHAU KULETA MREJESHO

ULIZA PALE AMBAPO HUJAELEWA KUPITIA COMMENT

Usisahau kulike na kushare

Address

Zanzibar City
71000

Opening Hours

Monday 07:00 - 18:00
Tuesday 07:00 - 18:00
Wednesday 07:00 - 18:00
Thursday 07:00 - 18:00
Friday 07:00 - 18:00
Saturday 07:00 - 18:00
Sunday 07:00 - 18:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Zanzibar Quality bakery posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Restaurant

Send a message to Zanzibar Quality bakery:

Share

Category