Kuku_Mkombozi

Kuku_Mkombozi Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Kuku_Mkombozi, Chicken Joint, Mahina-Kanyerere, Mwanza.

29/11/2023

Mzigo upo chap chap
Kuku wanauzwa
Bei ya jumla ni 16000/- tetea, jogoo 18000/- chap chap.
Tupo: Mwanza mkuyuni
0788313986

Tunauza mayai ya kuku chotara (kuroila)๐ŸฅšMayai yanafaa kwa kutotolesha na hutotolewa kati ya 95% na100% ya mayai yote ๐Ÿฃ๐Ÿฅšy...
28/05/2023

Tunauza mayai ya kuku chotara (kuroila)
๐ŸฅšMayai yanafaa kwa kutotolesha na hutotolewa kati ya 95% na100% ya mayai yote ๐Ÿฃ
๐Ÿฅšyanafaa kwa matumizi ya nyumbani (kula) ๐Ÿณ yanakiini cha njano 100%
๐Ÿ’ธBei ya tray ni 15000/-
๐Ÿ“Tunapatikana Mwanza.
๐Ÿ“žCall/sms/whatsapp 0788313986.
๐Ÿšš Tunasafirisha kwa gharama za mteja.

Karibuni sana

Kuku wetu Chotara aina ya kuroila wakiwa na miezi nane sasa. Kwa ushauri 0788313986
28/05/2023

Kuku wetu Chotara aina ya kuroila wakiwa na miezi nane sasa.
Kwa ushauri 0788313986

ULEAJI WA VIFARANGA.SEHEMU YA KWANZA ๐ŸคUleaji wa vifaranga ni kazi nyepesi sana lakini pia ni kazi ngumu mnoo.๐Ÿ‘‰๐ŸพMalezi ya...
27/05/2023

ULEAJI WA VIFARANGA.

SEHEMU YA KWANZA

๐ŸคUleaji wa vifaranga ni kazi nyepesi sana lakini pia ni kazi ngumu mnoo.

๐Ÿ‘‰๐ŸพMalezi ya vifaranga huanzia siku ya kwanza tangu kifaranga kianguliwa kutoka kwenye yai ambapo kazi hio hufanywa na kifaranga mwenyewe kwa kutoboa ganda la yai.

๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Kwa kawaida kifaranga kinapoanguliwa huweza kukaa muda wa masaa 72 bila ya kupata chakula chochote wala maji.

๐Ÿ‘†๐Ÿผ Haina maana kwamba uwaache vifaranga kwa saa 72 ndio uwape chakula la hasha unapaswa kufanya haya ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ

โšซ Siku ya kwanza
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kupokea vifaranga (brooder) inapaswa kuwekewa maji na joto la kutosha kwa muda wa walau masaa mawili hadi matatu ili vifaranga wasipate baridi pindi wanapofika na maji yaweze kutoa ule ubaridi na kuwa vugu vugu

๐Ÿ‘‰๐Ÿพ K**a vifaranga vimetoka mbali hufika bandani wakiwa wamechoka hivyo unapaswa kuwawekea maji yaliyochanganywa na glucose kwa muda wa walau masaa mawili kisha unaweza wapatia chakula

โŒ Usiwape chakula moja kwa moja maana mfumo wa mzunguko wa damu unakua juu sana hivyo inaweza pelekea shida kwenye kuweza kujua kiwango stahili cha chakula na kifaranga kula sana na hatimae kufa

๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Wapatie chakula aina ya starter kwenye vyombo ambavyo ni vipana k**a vile sinia au benesi zenye kuinuko mfupi sana. Weka vyombo vingi ili kila kifaranga apate nafasi ya kula vizuri

๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Pindi wafikapo ndani ya brooder angalia muitikio wao ili kujua vifaranga walioathirika zaidi ili uweze kuwasaidia kwa namna moja au nyingine

๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Ifahamike kwamba kifaranga hakifahamu kitu chochote kile kipindi kinatotolewa hivyo unapaswa kukielekeza baadhi ya vitu mfano kunywa maji ili kisiingie ndani ya chombo cha maji kikaloana kwa kufanya hivyo itafanya vifaranga wengi wafundishane namna ya kunywa maji

Sehemu ya pili itaendelea.....

*kuku ni mkombozi wa kiuchumi. Anza kufuga kuku acha kuishi na kuku*

๐Ÿ‘‰๐Ÿพ Kwa ushauri kuhusuana na kuku
๐Ÿ“ž 0788313986, 0766641405
๐Ÿ“ Mwanza

*EPUKA MAGONJWA YA KUKU* *Sehemu ya mwisho*โœ๐Ÿพ Usitunze vitu ndani ya banda wala uchafu k**a vile majani yaliyokauka. Waf...
21/04/2023

*EPUKA MAGONJWA YA KUKU*

*Sehemu ya mwisho*

โœ๐Ÿพ Usitunze vitu ndani ya banda wala uchafu k**a vile majani yaliyokauka. Wafugaji wengi tunatabia ya kutunza vyombo vya maji na chakula ( *ambavyo havitumiki au vimeharibika* ) ndani ya banda au kutunza kitu chochote ambacho hakitumiki k**a boksi kitu ambacho hupelekea kuwavutia wanyama wadogo k**a panya kutengeneza makao. Vile vile inaweza kupelekea kuzaliana kwa wadudu k**a mbu ambao kwa namna moja au nyingine wanasambaza baadhi ya magonjwa k**a vile ndui ( *k**a vile malaria inavyosambaza kwa binadamu)* hivyo epuka kutunza vitu ndani ya banda.

โœ๐Ÿพ Safisha banda la kuku mara kwa mara kupunguza au kuzuia kuzaliana kwa mayai ya minyoo na bakteria. Kwa wale wafugaji wanaotumia vizimba ( *cages* ) hakikisha unaweka ratiba nzuri ya kufanya usafi mahali kinapoangukia kwani kwa kufanya hivyo unapunguza uwezekano wa kuzaliwa kwa bakteria na minyoo ambao wanaweza athiri mazingira yanayozunguka banda la kuku

โœ๐ŸพSafisha kwa dawa mashine ya kutotoleshea ( *Incubator* ) kabla naa baada ya kuitumia. Magonjwa yanaweza kuambukizwa pia kupitia Incubator kipindi cha utotoleshaji hivyo mfugaji unapaswa kusafisha mashine ya kukutoleshea vifaranga kwa dawa

โœ๐Ÿพ Tunza kumbukumbu ya matukio yote yanayoendelea kwa kuku wako. Hapa wengi wetu tunafanya kwa mazoea tu kitu ambacho kinapelekea kukwama kiuchumi.
๐Ÿ‘†๐Ÿผ Tunza kumbukumbu ya vitu k**a mayai yaliyotagwa, chakula kilichotumika, vifo vya kuku, wageni waliofika bandani, chanjo na afya ya kuku kwa ujumla.

โœ๐Ÿพ Usiruhusu maji kutuama bandani kwani hupelekea mazalia ya mbu na kuku wanaweza kunywa na kupata magonjwa ya tumbo

โœ๐Ÿพ Wapatie kuku chakula chenye virutubisho vyote na Wapatie kwa kiwango sahihi (pima kiwango cha chakula kwa kuku *120gm-125gm* kwa kuku wakubwa kwa siku kulingana na mchanganyiko) Wapatie chakula kwa wakati maalumu ( *soma sehemu ya kwanza* )

โœ๐Ÿพ Wapatie sehemu ya kivuli kwa ajili ya kupumzika.

โœ๐Ÿพ Punguza mwanga kwenye viota kwani kuku wanahitaji usiri na sehemu iliyojifika ili kutaga pia hupunguza kishawishi cha kula mayai endapo pakiwa wazi

โœ๐Ÿพ Wapatie kuku vichanja ikumbukwe kuwa kuku nao ni ndege k**a ilivyo kwa ndege pori wanapenda kulala juu kwani wanajisikia usalama mkubwa zaidi pindi wanapolala juu tofauti na wakilala chini. Hivyo wawekee vichanja ambavyo wanaweza kusimama na walau kukunja vidole vyo kuzunguka hii hupelekea kuwapa mazoezi.

๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“

*KUKU NI MKOMBOZI WA KIUCHUMI KWA RIKA ZOTE*

๐Ÿ‘‰๐Ÿป Karibu kwa ushauri, ujenzi wa banda na kutembelea mashamba ya kuku

๐Ÿ‘‰๐Ÿป Brightfame
๐Ÿ“ž 0788313986, 076641405
๐Ÿ“ Mwanza

*MWANZA MWANZA!* Tumeshusha bei za mayai ya kuku wote ( *kienyeji na chotara* )Bei ni k**a ifuatavyo kwa sasa  ๐Ÿ‘‰๐Ÿพ *Kwa a...
18/04/2023

*MWANZA MWANZA!*

Tumeshusha bei za mayai ya kuku wote ( *kienyeji na chotara* )

Bei ni k**a ifuatavyo kwa sasa
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ *Kwa ajili ya kula ni 13000-*
๐Ÿ‘‰๐Ÿพ *kwa ajili ya kutotolesha (15000)*

๐Ÿ‘†๐Ÿผ Discount ipo kuanzia trey 5.
๐Ÿ“ Tupo mwanza mkuyuni

๐Ÿ“ž Call/sms 0788313986

Delivery ipo Kwa gharama za mteja

*EPUKA MAGONJWA YA KUKU*.. *Sehemu ya pili*โœ๐Ÿพ Ondoa vyakula vilivyosalia  kwenye vyombo ambavyo kuku hawajala. Kuna wany...
14/04/2023

*EPUKA MAGONJWA YA KUKU*
.. *Sehemu ya pili*

โœ๐Ÿพ Ondoa vyakula vilivyosalia kwenye vyombo ambavyo kuku hawajala. Kuna wanyama wa mbali mbali wadogo ambao nao wanakula vyakula k**a pumba, mahindi n.k mfano wa wanyama hao ni panya, wadudu k**a siafu ambao wanaweza kua na madhara kwa kuku k**a vile kuwajeruhi. _Vilevile mrundikano wa vyakula unaweza tengeneza sumu_ *(mycotoxin)* hususani vile vyenye asili ya mbegu k**a soya.

โœ๐Ÿพ Toa na zika ( *choma moto* ) mbali mara moja kuku waliokufa. Endapo kuku atakufa ndani ya banda ni vizuri umtoe na umzike mbali ili asiweze kuwaambukiza wenzake ( *k**a chanzo cha ugonjwa unajua)*
K**a chanzo cha ugonjwa hakijulikani muite mtaalamu wa wanyama akusaidie kwa msaada zaidi au fika maabara ya wanyama iliyokaribu nawe kwa vipimo zaidi.

โœ๐ŸพSafisha mikono yako kabla na baada ya kuwahudumia kuku. Ifahamike kwamba kuna baadhi ya magonjwa yanaweza kuambukizwa kutoka kwa kuku kwenda kwa binadamu k**a vile salmonella ( *mfano typhoid* ) ambapo watoto na wazee huathirika zaidi. Hivyo nawa mikono kabla na baada ya kuwahudumia kuku ili kuzuia kusafirisha magonjwa kutoka kwa kuku kwenda kwa binadamu

โœ๐Ÿพ Usiwabananishe kuku kwenye eneo dogo. Kuku wanahitaji kufanya mazoezi ya viungo k**a ilivyo kwa binadamu k**a vile kukimbia, kunyoosha mabawa wape kuku nafasi ya kutosha walau mita 1 ya mraba kwa kuku watano. Vilevile kuwabananisha kuku hupelekea ukuaji hafifu wa kuku kutokana na stress. Wape kuku uhuru na nafasi ya kutosha

โœ๐Ÿพ Usiazime wala usichanganye vyombo vya kuku. Usiazime vyombo vya kuku kutoka kwa mfugaji mwenzako nawe ukaanza kuvitumia mara moja kwani vinaweza kuwa vimebeba magonjwa kutoka banda husika, na usichanganye vyombo kutoka banda moja kwenda lingine kwani vinaweza kusababisha kusambaza ugonjwa endapo utatokea kwa kundi mojawapo ya kuku wako au ndege ulionao. *K**a hilo halizuiliki hakikisha unavisafisha kwa dawa nzuri ya kuuwa vimelea vya magonjwa*
๐Ÿ‘†๐Ÿผjapo si salama

โœ๐Ÿพ Vyombo vya chakula na maji vinapaswa kusafishwa na dawa mara kwa mara. Mara nyingi unapotumia dawa au vitamini kwenye maji hupelekea kuganda kwenye kingo za vyombo kitu ambacho baada ya muda hupelekea kutengenezeka kwa fungasi ambazo zinaweza sababisha magonjwa k**a kolibasilosisi na konsidiosisi ( *collibasilosis, coccidiosis* ) . Ni vyema vyombo hivi vikasafishwa na dawa ya kuua fangusi kila baada ya muda fulani k**a wiki 2 hadi 3 ama kadili utakavyoweza. Unaweza kutumia jik k**a chombo ni cheupe ama V-rid k**a biosecurity

โœ๐Ÿพ Badilisha matandiko mara yanapochafuka. Kwa wale ambao wanafuga kuku kwenye sakafu ni vizuri kuwawekea matandiko k**a vile pumba za mpunga au maranda walau unene wa sentimita 5-7 na kuyageuza mara kwa mara pindi yanapochafuka. Endapo yakijaa yaondolewe mara moja kwani yanapelekea kutengenezeka kwa harufu kali ya Amonia ambayo huweza kusababisha mafua kwa kuku.

๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“

Kuku ni mkombozi wa kiuchumi. Anza kufuga kuku acha kuishi na kuku.

๐Ÿ‘‰ Kwa ushauri, ujenzi na kutembelea mashamba ya kuku
๐Ÿ“ž 0788313986, 0766641405
๐Ÿ“ Mwanza.

*EPUKA MAGONJWA YA KUKU* *Sehemu ya kwanza*โœ๐Ÿพ Usichanganye ndege wa aina tofauti ( *mfano kuku,kaka,Bata n.k* ) kwenye b...
12/04/2023

*EPUKA MAGONJWA YA KUKU*

*Sehemu ya kwanza*

โœ๐Ÿพ Usichanganye ndege wa aina tofauti ( *mfano kuku,kaka,Bata n.k* ) kwenye bando moja. Hii inaweza kuwa sababu ya kuanza kudonoana (cannibalism) kulingana na mahitaji tofauti tofauti ya kila aina ya ndege.

โœ๐Ÿพ Usichanganye kuku wa umri tofauti pamoja ( *mfano kuku wanaokua na kuku wanaotaga*). Kwanza italeta changamoto kwenye kuwalisha kwa sababu kila umri wa kuku unaaina yake ya chakula ( _tutaona kwenye somo la chakula_ )
Pili, ukuaji duni wa kuku wadogo kwani mara zote watakua wakionewa na kuku wakubwa hususani kudonolewa na hivyo kuwa chanzo cha kudonoana kuku

โœ๐Ÿพ Usichanganye kuku wagonjwa na wasio wagonjwa.
Hii inasaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa kutoka kwa kuku wagonjwa kwenda kwa kuku wenye ( *k**a ni ugonjwa wa kuambukiza* ).
Kuku wagonjwa watengwe mbali na kuku wenye afya.

๐Ÿ‘†๐Ÿผ unapotaka kuhudumia anza na kuku wazima kisha [k**a mazingira yanaruhusu badilisha mavazi] hudumia kuku wagonjwa ili kuepuka kusambaza magonjwa

โœ๐Ÿพ Weka karantini kuku wapya. Unaponunua kuku wapya usiwachanganye moja kwa moja na kuku waliopo bandani. Kuku wapya huenda wakawa na wamebeba vimelea vya magonjwa mbali mbali k**a vile tyhoid *hata k**a hawaoneshi dalili za ugonjwa*
Hivyo kuku wapya watengwe [waleke karantini] walau kwa wiki 2 kabla ya kuwachanganya na wengine.

โœ๐Ÿพ Usiruhusu watu kuingia bandani bila utaratibu. Weka utaratibu wa namna watu wanavyoweza kuingia bandani ikiwa ni pamoja na kuweka vitakasa mlangoni {foot path} au [ *kuwa na mavazi maalumu k**a itafaa]*
๐Ÿ‘†๐Ÿผ Watu wanaweza kubeba vimelea mbali mbali vya magonjwa kupitia viatu au nguo kutoka sehemu moja kwenda nyingine

โœ๐Ÿพ Usiweke vyombo vya chakula nje wanapofika ndege aina zote. Ifahamike kwamba ndege pori nao wanapata magonjwa mbalimbali k**a ya kuku, hivyo usiweke vyombo vya chakula mahali ambapo patawavutia ndege pori kuja kula kwani baadhi yao wanaweza kuleta magonjwa kwa kuku na wengine wanaweza kuwadhuru kuku.

โœ๐Ÿพ Tengeneza uzio. Ili kuepuka muingiliano wa watu au vitu visivyoruhusiwa watengenezee kuku wako uzio ili kuwalinda dhidi ya maadui mbali mbali k**a wanyama wakali k**a vile paka, kenge wanaoweza kuwadhuru.

*Sehemu ya pili itaendelea.......*

๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“
Kuku ni mkombozi wa kiuchumi. Fuga kuku acha kuishi na kuku

๐Ÿ‘‰ Kwa ushauri, ujenzi na kutembelea mashamba ya kuku
๐Ÿ“ž 0788313986, 0766641405
๐Ÿ“ Mwanza

Tunauza mayai ya kuku wa kienyeji๐ŸฅšMayai yanafaa kwa kutotolesha ๐Ÿฃ๐Ÿฅšyanafaa kwa matumizi ya nyumbani (kula) ๐Ÿณ๐Ÿ’ธBei ya tray ...
09/04/2023

Tunauza mayai ya kuku wa kienyeji
๐ŸฅšMayai yanafaa kwa kutotolesha ๐Ÿฃ
๐Ÿฅšyanafaa kwa matumizi ya nyumbani (kula) ๐Ÿณ
๐Ÿ’ธBei ya tray ni 13000/-
Tunapatikana Mwanza.
Call/sms/whatsapp 0788313986.
Delivery ipo kwa gharama za nafuu.
Karibuni sana

Tunauza mayai ya kuku chotara (kuroila)๐ŸฅšMayai yanafaa kwa kutotolesha ๐Ÿฃ๐Ÿฅšyanafaa kwa matumizi ya nyumbani (kula) ๐Ÿณ๐Ÿ’ธBei ya...
15/01/2023

Tunauza mayai ya kuku chotara (kuroila)
๐ŸฅšMayai yanafaa kwa kutotolesha ๐Ÿฃ
๐Ÿฅšyanafaa kwa matumizi ya nyumbani (kula) ๐Ÿณ
๐Ÿ’ธBei ya tray ni 14000/-
Tunapatikana Mwanza.
Call/sms/whatsapp 0788313986.
Delivery ipo kwa gharama nafuu sana
Karibuni sana

๐Ÿ“ Tunauza mayai ya kienyeji hasili๐ŸฅšMayai yetu yanafaa kwa kutotoleshea na matunizi ya nyumbani๐Ÿ’ฐTrey moja tunauza sh 1400...
16/12/2022

๐Ÿ“ Tunauza mayai ya kienyeji hasili

๐ŸฅšMayai yetu yanafaa kwa kutotoleshea na matunizi ya nyumbani

๐Ÿ’ฐTrey moja tunauza sh 14000/-

โœ… Tunapatikana Mahina kanyerere Mwanza

๐Ÿ“žCall/sms/Whatsapp 0788313986

๐ŸฃTunauza vifaranga vya kuku wa nyama (BROILER)Call/sms/Whatsapp 0788313986๐ŸฃKuku hawa wanakua haraka na hufikia uzito wa ...
22/11/2022

๐ŸฃTunauza vifaranga vya kuku wa nyama (BROILER)

Call/sms/Whatsapp
0788313986

๐ŸฃKuku hawa wanakua haraka na hufikia uzito wa kg 1.5 ndani ya siku 21
๐ŸฃBei ya kifaranga ni 2100/-
Tunapatikana Mwanza mahina kanyerere

๐ŸฃKaribu kuweka order yako mapema
0788313986

Address

Mahina-Kanyerere
Mwanza

Opening Hours

Monday 07:00 - 20:00
Tuesday 07:00 - 20:00
Wednesday 07:00 - 20:00
Thursday 07:00 - 20:00
Friday 07:00 - 20:00
Saturday 07:00 - 20:00
Sunday 10:00 - 20:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kuku_Mkombozi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category