Save Wild Uyoga

Save Wild Uyoga Fleshy Mushrooms

29/10/2019

TUNATANGAZA NAFASI ZA KAZI KATIKA NGAZI ZIFUATAZO ASSISTANT MUSHROOM PROJECT FACILITATOR –Nafasi 1 Sifa za

Kwa ushauri na mafunzo kuhusu kilimo cha Uyoga wasiliana nasi kwa namba 0755558837, 0784359492. Pia unaweza tembelea ofi...
05/10/2019

Kwa ushauri na mafunzo kuhusu kilimo cha Uyoga wasiliana nasi kwa namba 0755558837, 0784359492. Pia unaweza tembelea ofisi zetu zilizopo Manispaa ya Morogoro mjini, mtaa wa Mtoni. Picha Chini inaonesha uandaaji wa mashamba ya Uyoga.


MAPISHI YA UYOGA:UYOGA "ROSTI";Mahitaji:Uyoga-200gram Viungo: Nyanya, Kitunguu maji, Karoti, Pili Pili hoho, Kitunguu sw...
28/02/2019

MAPISHI YA UYOGA:
UYOGA "ROSTI";
Mahitaji:
Uyoga-200gram
Viungo: Nyanya, Kitunguu maji, Karoti, Pili Pili hoho, Kitunguu swaumu na viungo vingine upendavyo na kadiri utakavyoona inafaa.
Mafuta- kijiko kimoja(sio lazima)
Chumvi- kiasi
Matarisho:
Baada ya kuandaa viungo vyako; weka mafuta kiasi kaanga vitunguu na viungo vyako k**a unaunga nyama.
Baada ya viungo vyako kuiva weka uyoga uliouchambua au kukatakata vipande vya wastani, baada ya dk 20-25: " Rosti" yako itakuwa tayari.
Unaweza kula na wali,ugali, na chochote utakachopenda k**a mboga ya kawaida; ni mtamu sana!
Muhimu:
Jenga tabia ya kula Uyoga Mara kwa Mara kwani ni mzuri kiafya, una vitamini, madini mengi na husaidia kutibu maradhi mbalimbali; wazoeshe watoto kula uyoga kwani una protini nyingi ambayo husaidia ukuaji na madini k**a Calcium husaidia afya ya mifupa na akili.
Kwa mahitaji ya Uyoga fresh kutoka shambani wasiliana na ECOWICE, piga Simu namba 0755558837, 0744490122.
Tupo Mkoani Morogoro, Mtaa wa Mtoni.
KARIBU SANA.

UVUNAJI WA UYOGAUyoga huwa tayari kuvunwa siku tatu baada ya vichwa kuonekana. Uyoga uvunwe kwa mkono kwa kushika katika...
21/02/2019

UVUNAJI WA UYOGA

Uyoga huwa tayari kuvunwa siku tatu baada ya vichwa kuonekana. Uyoga uvunwe kwa mkono kwa kushika katikati ya shina la uyoga, kisha zungusha hadi uyoga ung’oke. Usiondoe kichwa peke yake katika kuvuna uyoga kwani kubakiza shina huzuia uyoga mwingine kutokea.

Uyoga hufanya damu kuwa nyepesi, unazuia saratani, unashusha kiwango cha kolestro, huchangamsha mfumo wa kinga ya mwili ...
20/02/2019

Uyoga hufanya damu kuwa nyepesi, unazuia saratani, unashusha kiwango cha kolestro, huchangamsha mfumo wa kinga ya mwili na hudhoofisha virusi.

FAHAMU KUHUSU AINA TOFAUTI ZA UYOGASHIMEJIUyoga huu ni mahususi kwa kupambana na asthma, uvimbe. Uyoga huu una kemikali ...
18/02/2019

FAHAMU KUHUSU AINA TOFAUTI ZA UYOGA

SHIMEJI
Uyoga huu ni mahususi kwa kupambana na asthma, uvimbe. Uyoga huu una kemikali aina ya beta-glucans ambayo kwa mujibu wa taasisi ya kansa ya japani (Japan National Cancer Institute) kemikali hii imesaidia kuondoa vimbe zilizosababishwa na kansa. Pia uyoga huu husaidia watu wenye kisukari,na alegi mbalimbali.

NAMNA YA KUPANDA UYOGAKuna aina mbili za upandajiAina ya kwanzaChukua mfuko wa nailoni wenye upana wa cm 40 – 45 na kimo...
15/02/2019

NAMNA YA KUPANDA UYOGA

Kuna aina mbili za upandaji

Aina ya kwanza

Chukua mfuko wa nailoni wenye upana wa cm 40 – 45 na kimo cm 75. Weka tabaka la mali ghafi ya kuoteshea yenye kina cha sm 10 katika mfuko halafu tawanya mbegu ya uyoga juu yake. Baada ya kuweka mbegu, weka tena tabaka nyingine ya vioteshea na kuweka mbegu juu yake. Endelea kuongeza tabaka kwa namna hii mpaka ifike ujazo wa robo tatu ya mfuko.

Aina ya Pili

Changanya malighafi ya kuoteshea (baada ya kuchemshwa na kupoa) na mbegu ya uyoga katika uwiano wa 1: 25 (mbegu : malighafi ya kuoteshea) kwa uyoga aina ya mamama (Pleurotus spp.). Kisha mchanganyiko huo ujazwe katika mifuko ya nailoni mifuko hii iwe na ukubwa wa cm 20 kwa cm 40 ambamo unaweza kujaza kilo 1 – 1.5 ya mali ghafi ya kuoteshea.

Funga mifuko na toboa matundu kwenye mifuko yenye kipenyo cha cm 1 kwa kila umbali wa cm 6 hadi 10 kwa kila mfuko.Matundu yawe mengi ili kuingiza hewa ya kutosha ndani ya mifuko. Kumbuka uyoga ni kiumbe hai hivyo unahitaji kupumua.

FAHAMU KUHUSU AINA TOFAUTI ZA UYOGAPORCINIUyoga huu huweza kuzuia uvimbe na kutokea k**a kansa na majipu kwa sababu ya k...
08/02/2019

FAHAMU KUHUSU AINA TOFAUTI ZA UYOGA

PORCINI
Uyoga huu huweza kuzuia uvimbe na kutokea k**a kansa na majipu kwa sababu ya kemikali iitwayo ergosterol ambayo huweza kuziharibu seli zote ziletazo madhara pamoja na kuua wadudu wanaoshambulia seli za mwili.

FAHAMU KUHUSU AINA TOFAUTI ZA UYOGASHIITAKEHuweza kupambana na kuponya uvimbe wa kila aina. Uyoga huu una kemikali iitwa...
04/02/2019

FAHAMU KUHUSU AINA TOFAUTI ZA UYOGA

SHIITAKE
Huweza kupambana na kuponya uvimbe wa kila aina. Uyoga huu una kemikali iitwayo lentinan ambayo hupambana na visababishi vyote vya uvimbe, wajapani wameanza kuitumia katika matibabu ya kansa.


UYOGA NA UHIFADHI WA MAZINGIRAKilimo cha uyoga ni njia mojawapo ya kuhifadhi mazingira yetu kwasababu zifuatazo;1.Hulimw...
26/01/2019

UYOGA NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
Kilimo cha uyoga ni njia mojawapo ya kuhifadhi mazingira yetu kwasababu zifuatazo;

1.Hulimwa kwa kutumia masalia mbalimbali ya mazao k**a; maranda ya mbao, Maganda ya alizeti, karanga, miwa, maharage, Majani ya mpunga, mikunde, ngano. Hii hupunguza uchafu ambao ungetupwa au kuchomwa na kuchafua mazingira.

2. Baada ya kuvuna Uyoga masalia ya kimeng'enywa hutumika k**a mbolea nzuri kwa ajili ya mazao mbalimbali hasa bustani ya mboga mboga , pia masalia hayo hutumika kwa ajili ya kulishia wanyama mbalimbali.
Kwa mahitaji ya Uyoga, mbegu za Uyoga n.k pia mafunzo ya kuzalisha Uyoga kibiashara, wasiliana nasi 0755558837, 0784359492, Email: [email protected]

FAHAMU KUHUSU AINA TOFAUTI ZA UYOGAMAITAKEHufahamika kwa umaarufu wake wa kuzuia na kuponya kansa ya matiti kwa wanawake...
25/01/2019

FAHAMU KUHUSU AINA TOFAUTI ZA UYOGA

MAITAKE
Hufahamika kwa umaarufu wake wa kuzuia na kuponya kansa ya matiti kwa wanawake ambayo huchochea kinga ya mwili na kusababisha kuuwawa kwa seli za kansa.


FAHAMU KUHUSU AINA TOFAUTI ZA UYOGAREISHIUyoga huu huweza kupambana kwa kiasi kikubwa sana na bacteria ,virusi na kuvu a...
23/01/2019

FAHAMU KUHUSU AINA TOFAUTI ZA UYOGA

REISHI

Uyoga huu huweza kupambana kwa kiasi kikubwa sana na bacteria ,virusi na kuvu au fangasi. Pia uyoga huu huweza kuzuia kutokea kwa kansa. Uyoga una kemikali iitwayo gandodermic acid ambayo huweza kupunguza na hatimaye kuondoa mafuta mabaya mwilini na kurekebisha shinikizo la damu mwilini.


Address

Morogoro

Opening Hours

Monday 08:00 - 17:00
Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00
Thursday 08:00 - 17:00
Friday 08:00 - 17:00
Saturday 08:00 - 17:00

Telephone

+255 755 558 837

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Save Wild Uyoga posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Restaurant

Send a message to Save Wild Uyoga:

Share

Category