12/11/2023
Mwafrika anasafiri kwenda Israel kufanya maombi kwenye ukuta uitwao western Wall. Wakiristu hufika na kusali. Maombi mengine huandikwa kwenye karatasi na hubandikwa kwenye huu ukuta kwa imani kuwa maombi yao yamefika kwa Muumba. Mkristu aliefika huko hupewa cheo cha u-JP, yaani mahujaji. Mwafrika, muislam hufanya vile vile, husafiri hadi Saudi Arabia kusali juu ya jiwe jeusi, huko huitwa HIJa na aliefika hupewa cheo na kuitwa Alhaji.
Bali Mwafrika, anaesafiri kwenda kwenye asili yake alikozaliwa yeye au wazazi wake, ambako ndiko chimbuko la uzao wa ukoo wake, akienda KUSALI kwa asili ya babu zake k**a kwenye Jiwe, Mto, Mti au walimozikwa mababu zake, kwa imani ya kwao, hawa watu TUNAWAITA WAPAGANI, Wanabudu MIZIMU, Ni washirikina nk. Kwa mfano wachagga huambiwa wameenda kutambika, kitu ambacho pia wengi huchanganya KUTAMBIKA NA KUCHAWIA. Ila aliesafiri kilometer 8000 kwenda kuongea sala zake mbele ya jiwe na kuweka maombi ya kuandikwa kwenye mianya ya jiwe pale Israel, YEYE HAJATAMBIKA. Duu.
Huu ni Utumwa wa Akili ambao tunapitia waafrika, kudhani chochote cha MZUNGU ndo sahihi, ila cha mwafrika ni cha kishetani... HUU NI UTUMWA WA AKILI, AMBAO ni mkubwa kushinda utumwa wa kikoloni.
Kila Kabila au Taifa lina kiini chao cha Kipekee cha mawasiliano, cha kuabudu, kilicho asisiwa na Wahenga Wao Wenyewe. Na ni haki kabisa kuenzi na kuamini hayo mapokeo. Sasa sisi tunaacha asili yetu, tunaenda kuabudu ya Muisrael. Muisrael mwenyewe yuko kwenye vita kubwa na Ndugu yake Mpalestina, anatumia Mabomu na Maroketi kupigana..... Na sisi huku tuko bize kumuomba mungu wa Israel atusaidie.
Kuna shida kubwa.
Imetafsiriwa na GPM