13/11/2020
KOSA KUBWA LINALOFANYWA NA WAFUGAJI WENGI BILA KUJUA.
Masomo mengi ya utoaji chanjo kwa kuku yamekuwa yakieleza ratiba za utoaji chanjo bila ya kusisitiza jambo muhimu zaidi ambalo ni matumizi sahihi ya chanjo husika.
Hapa nazungumzia chanjo zinazochanganywa na Maji. (Oral Live Vaccines). eg. Newcastle, Gumboro (IBD) etc.
Kutokana aina za chanjo tajwa hapo juu zinahitajika kuchanganywa na maji ndipo uwapatie kuku kwa muda usiozidi masaa mawili, basi wafugaji wengi hatufahamu kuwa si Kila maji unaweza kuchanganya na chanjo hizo.
Hapa nazungumzia maji ya Bombani. Ikumbukwe kuwa maji mengi ya bombani hasa kipindi hiki huwa yanakuwa treated/yanatibiwa/yanawekwa dawa ili kuhakikisha mtumiaji anapata /kunywa maji safi na salama.
Hivyo utakapoyatumia wewe mfugaji kwa ajili ya kuchanganya na chanjo itapelekea chanjo yako kutokuwa kamilifu kiutendaji kazi (inefficiency) kutokana na maji uliyotumia tayari yana dawa ya kutakasa maji haswa Chlorine ambayo inakinzana na utendaji kazi wa chanjo uliyochanganya.
In short ni kwamba, pendelea kutumia maji safi ya Kisima, Mvua ama maji yasiyokuwa na chlorine/ambayo hayajaekwa dawa.
Ila sasa, kutokana na maeneo mengi ni ngumu kupata maji hayo.! itakupasa utumie dawa za Dechlorination uchanganye na maji ya bomba kwanza ili kutoa chlorine iliyochanganywa kwenye maji hayo ndipo uyatumie kuchanganya na chanjo uliyoiandaa.
Baadhi ya wafugaji huchemsha maji yao kabla ya kuyatumia kwa ajili ya chanjo lakini niwashauri tu wafugaji wenzangu kuwa, ukichemsha maji huondoi chorine kwenye maji labda kwa kiasi fulani tuu, ila kwa uhakika zaidi itakubidi uyachanganye maji hayo na maziwa ya Unga (Milk powder). Ingredients za milk powder husaidia kuondoa chlorine kwenye maji k**a njia m,badala ya kutumia dawa special kwa ajili ya dechlorination.
Niishie hapo kwa leo, ila k**a una swali ama ushauri tucheki kupitia namba zetu. 0783-554005 (Call/Whatsapp/Txt)
Tupo Mbeya Tunduma
0746090774