12/03/2023
Amani Ya Mola Iwe Juu Yenu
Kwanini Tunaghairisha Kuanza Ufugaji...(SEHEMU YA PILI)
🗣️Tuseme kwa pamoja Nitaanza kidogo kidogo ili nitimize malengo yangu...Hayaa Turudie tenaaa
🗣️Nitaanza kidogo kidogo ili nitimize malengo yangu...
🚨Kuna Mda Tumekua Tukichelewa Kuchukua Maamuzi Ya Kuanza Ufugaji kwasababu Ya Mihemko Ya Kutaka Kuanza Kufuga Kwa Ukubwa Ulio Nje Ya Uwezo Wetu...
✍️Tuelewane Kidogo Kuanza Ufugaji Na Mtaji Mkubwa Sio Vibaya Ila Ni Vizuri Zaidi Kuanza Na Ufugaji Mdogo Atak**a Unamtaji Mkubwa...
🛑Tumekua tukijipa pressure kubwa kwasababu ya Kutaka Kuanza hatua kubwa...
Swali..???
🤔Kwanini ujipe pressure kwa kuanza Ufugaji mkubwa wakati unaweza ukaanza na ufugaji wa mtaji wa kawaida halafu ukakufikisha uko unakotaka ufike...???
🥳KWANINI NASHAURI WATU WAANZE NA UFUGAJI WA KAWAIDA(MDOGO)
✍️ Kwanza Hii itakusaidia uachane na tabia ya kughairisha,,,, nitaanza kesho... sijui mwezi ujao... sijui mwaka ujao... kwasababu watu wengi wameghairisha kuanza ufugaji kwakulazimisha kutafuta mtaji mkubwa ili aanze ufugaji mkubwa jambo ambalo sio sahihi...❌
✍️Pia kuanza na Ufugaji Mdogo itakusaidia kukupa nguvu kwasababu utajifunza mengi kupitia huo ufugaji mfano soko lipoje...wateja wanahitaji nini... Jinsi ya kufata utaratibu wa chanjo... ni mda gani sahihi wa kununua vifaranga kwaajili ya kuja kuwakuza na kuwauza kwa siku sijazo... N.k kuliko kuanza na Mtaji Mkubwa ambao ukipata changamoto inaweza sababisha usifuge tena..😥
✍️Na pia itakusaidia kufuga bila pressure yoyote chukua Dk moja tu jaribu kuwaza aliyeanza ufugaji mkubwa na aliyeanza na ufugaji mdogo nani atakua kwenye pressure kubwa ya kuwaza..🥳
🎯Maneno yangu sio Sheria ila k**a wewe ni miongoni mwa watu wanaochelewa kuchukua Maamuzi ya kufuga kwasababu ya Kutaka Kuanza kwa Ukubwa my friend unajichelewesha kuanza safari ya kutimiza ndoto zako...
🎉🎉Tuanze kidogo kidogo itatupa hamasa,itatupa ujasiri,tutajifunza mengi, na pia itatupa uzoefu wa kufanya kwa Ukubwa Zaidi...
😘NA KIKUBWA ZAIDI TUTATIBU TABIA YA KUGHAIRISHA KWASABABU KUANZA KIDOGO HAKUNA STRESS SANA🥰
🇹🇿 MBARIKIWE SANA 🙏
🇹🇿 DOMCITY FARMING CENTER
🇹🇿12 MAR 23