Moshi Agrovet

Moshi Agrovet Tunauza CFP,vifaa vya kuku, chanjo,dawa na vitamini za kuku. Hatuuzi vifaranga โŒ

Kwa wafugaji mnaotafuta Connectors kwa ajili ya mfumo wa maji tunazo dukani Moja ni buku yaani elfu 1 Pia tunazo C**kStr...
04/09/2026

Kwa wafugaji mnaotafuta Connectors kwa ajili ya mfumo wa maji tunazo dukani Moja ni buku yaani elfu 1 Pia tunazo C**k

Straight zipo @1000
Elbow zipo @1000
Stoper zipo @1000
T connector zipo @1000
C**k zipo @5000

๐Š๐š๐ฆ๐š ๐ฎ๐ง๐š๐ก๐ข๐ญ๐š๐ฃ๐ข ๐œ๐จ๐ง๐ง๐ž๐œ๐ญ๐จ๐ซ๐ฌ, ๐œ๐ฎ๐ฉ ๐ง๐ข๐ฉ๐ฉ๐ฅ๐ž๐ฌ, ๐ฐ๐š๐ฏ๐ฎ ๐ฐ๐š ๐ค๐ฎ๐ค๐ฎ ๐š๐ฎ ๐‚๐จ๐œ๐ค ๐ญ๐ฎ๐ฉ๐ข๐ ๐ข๐ž ๐ŸŽ๐Ÿ•๐Ÿ“๐Ÿ๐Ÿ—๐Ÿ๐Ÿ๐Ÿ๐Ÿ‘๐Ÿ ๐š๐ฎ ๐ŸŽ๐Ÿ•๐Ÿ๐Ÿ– ๐Ÿ๐Ÿ—๐Ÿ ๐Ÿ‘๐Ÿ•๐Ÿ–

Ukihitaji Fundi, Tunaye fundi ambaye tunafanya naye kazi.

Moshi Agrovet Tunapatikana Dodoma Majengo Sokoni pembeni ya ilipokuwa CRDB MAJENGO - Jengo la Sophia plaza ofisi namba 2๐Ÿ“

Tupo wazi Jumatatu mpaka Jumamosi, Jumapili hatufungui โœ…

Post km hz ndo hutisha watu hasa kwny suala la chakula. Starter kg 50 ni 98000 Kwa 95000 tena hapo co mjini kabisa na ha...
01/09/2026

Post km hz ndo hutisha watu hasa kwny suala la chakula. Starter kg 50 ni 98000 Kwa 95000 tena hapo co mjini kabisa na hapo Kuna broiler starter na layers starter

halafu Kuna ww unaleta bei ya juu kupita kiasi. Kwa mtu asiyejua lazima umpige vilivyo, hii co fair. Tangaza biashara kulingana na bei iliyopo sokoni hata ukizidisha iwe kidogo

Hyo bei ya chakula ni kubwa sn tena sn

MAJIBU๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ

Kwanza ningependa uelewe kuwa huyu mdau hapo juu anarejea bei zetu za CFP ya starter ambazo ni hizi hapa

CFP ya starter kilo 5 ni 18,000 inatoshea kuchanganya chakula kilo 100

CFP ya starter kilo 25 ni 80,000 inatoshea kuchanganya chakula kilo 500

Zingatia hizi ni CFP za starter sio starter yaani ni hivi CFP ya starter ni virutubisho vinavyotumika kuchanganya chakula cha vifaranga

Ukiwa na CFP unahitaji mahindi, soya kavu , mashudu ya alizeti na mafuta ya mboga kukamilisha chakula kamili

Kumjibu huyu mdau nakupa mfano wa chakula kilo 100 unahitaji

Mahindi kilo 52
Soya kavu kilo 32
Mashudu ya alizeti kilo 9
Mafuta ya mboga kilo 2 [Lita 2.26]
CFP ya starter kilo 5

Jumla kilo 100

Muhimu CFP sio chakula kuku ni virutubisho vinavyotumika kuchanganya chakula cha kuku

Tunapatikana Dodoma Majengo Sokoni

Mawasiliano 0752 912132 au 0718 192 378

Tunatarajia kupokea vifaranga 800 wa chotara tunawafuga kwa ajili ya nyama tutawauza wakiwa na miezi 2 [siku 60] , Je tu...
01/09/2026

Tunatarajia kupokea vifaranga 800 wa chotara tunawafuga kwa ajili ya nyama tutawauza wakiwa na miezi 2 [siku 60] , Je tutawaandalia stata kilo ngapi na grower kilo ngapi ?

A. stata kilo 300 na grower kilo 1800

B. stata kilo 800 na grower kilo 3600

C. stata kilo 800 na grower kilo 2500

D.stata kilo 400 na grower kilo 4000

Tupe jibu lako kwenye comment tujifunze pamoja ๐Ÿ‘

MAJIBU ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

VIFARANGA 800 WANAHITAJI STATA KILO 800 NA GROWER KILO 3600

Stata watakula kuanzia siku 1 mpaka siku 25 ambapo kifaranga mmoja anakula kilo 1 vifaranga 800 watakula chakula kilo 800

Grower watakula kuanzia siku 25 mpaka siku 60 ambapo kuuu mmoja anakula chakula kilo 4.5, kuku 800 watakula grower kilo 3600

Asante sana kwa usikivu wako kwenye hili suala.

1.Kuku chotara 200 wenye umri wa siku 28 kwa siku watakula chakula kilo ngapi?JIBU๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐ŸฝWatakula kilo 20.22.Kuku chotara...
31/08/2026

1.Kuku chotara 200 wenye umri wa siku 28 kwa siku watakula chakula kilo ngapi?

JIBU๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ
Watakula kilo 20.2

2.Kuku chotara 150 kuanzia siku 1 mpaka siku 60 watakula chakula kilo ngapi?

JIBU๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ
Watakula chakulia kilo 825

Fanya mambo haya Kujifunza zaidi...

1.Kwanza pakua hii chati ya kuku wa sasso ambayo utaitumia kujua kiwango cha chakula wanachokula kila siku kuanzia siku 1 mpaka siku 60

Kupakua hiyo chati bofya hii link hapa๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ

https://drive.google.com/file/d/1JyGNxKDUKYsQyaQAkHvE0KB-702M1Mhr/view?usp=drivesdk

๐Ÿ‘‰๐ŸฝK**a huwezi kupakua hii chati tafuta mtu akusaidie kuipakua na unaweza kwenda nayo stationery wakakuchapishia ukawa na nakala ngumu [hard copy]

๐Ÿ‘‰๐ŸฝChati hii ni ya sasso na tunaitumia kwa kuku chotara aina zote, hatuna chati za chotara wengine k**a unayo unaweza kuitumia.

2.Jambo la pili Jifunze kutumia hiyo chati kwa kuangalia hii video hapa kwa kubofya hii link ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ

https://youtu.be/ssrq3vHNL0o

๐Ÿ‘‰๐ŸฝK**a unapata changamoto kuangalia hii video tafuta mtu akusaidie namna ya kufungua hii video ya YouTube najua tunatofautiana!

3.Jambo la tatu hakikisha unawalisha kuku kwa kipimo kila siku k**a ambavyo hiyo chati inaonesha kiwango husika kwa kila siku

Hapa unahitaji mzani, k**a Bado huna mzani tupigie 0752 912132 kuagiza mzani wa kidijitali bei yake ni 20,000 na unapima kuanzia gram 100 mpaka kilo 50. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Moshi Agrovet tunapatikana Dodoma Majengo Sokoni

Zingatia kwamba kiwango cha chakula wanachokula kitakuwa kinabadilika kadri wanavyokua siku kwa siku

4.Ulishaji wa chakula ni asubuhi na mchana utagawa chakula nusu kwa nusu yaani k**a kuku wako chotara wanakula chakula kilo 20 kwa siku utawapa kilo 10 asubuhi na jioni utawapa kilo 10

๐€๐๐†๐€๐‹๐ˆ๐™๐Ž

Jifunze jinsi ya kuwalisha kuku wako kwa kufuata viwango vinavyoelekezwa kupitia hiyo chati

Tafadhali sisi hatutakufanyia hayo mahesabu ndio maana tumeandaa chati na hiyo video ili uweze kujifunza na kufanya wewe mwenyewe kila siku hapo bandani kwako.

Ni rahisi Wala sio ngumu

Asante sana kwa usikivu wako kwenye hili suala ๐Ÿ™๐Ÿฟ

CFP
Ulishaji wa uhakika

Kuku wanamaliza chakula mapema Nitafanyaje chakula kilo 5.5 kitoshee mpaka siku 60?๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐ŸฝHabari yako, leo nilipa...
31/08/2026

Kuku wanamaliza chakula mapema Nitafanyaje chakula kilo 5.5 kitoshee mpaka siku 60?

๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ

Habari yako, leo nilipata ugeni wa mama cheupe [sio jina halisi] huyu ni mteja wangu mzuri wa CFP za kuku wanaokua hapa Dodoma

Leo alikuja dukani na alikuwa ana changamoto yake ambayo ni hii "afanyaje chakula kitoshee mpaka siku 60" nilimpa ushauri wa nini Cha kufanya ili chakula kilo 5.5 kitoshee mpaka siku 60

Inawezekana huelewi hii dhana ya chakula kilo 5.5 imetokea wapi, usiwaze... Iko hivi mfumo wetu wa ulishaji wa kuku chotara umegawanyika sehemu mbili

Sehemu ya kwanza ni kuanzia siku 1 mpaka siku 25 ambapo kuku mmoja anakula chakula kilo 1 sehemu ya pili ni kuanzia siku 25 mpaka siku 60 ambalo kuku mmoja anakula chakula kilo 4.5

Kwahiyo kuanzia siku 1 mpaka siku 60 jumla kuku chotara mmoja anakula chakula kilo 5.5 si tumeelewana?

Sasa Ikiwa na wewe unapata changamoto hiyo ya chakula kilo 5.5 kutofika siku ya 60 Fanya mambo yafuatayo

1.Kwanza pakua hii chati ya kuku wa sasso ambayo utaitumia kujua kiwango cha chakula wanachokula kila siku kuanzia siku 1 mpaka siku 60

Kupakua hiyo chati bofya hii link hapa๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ

https://drive.google.com/file/d/1JyGNxKDUKYsQyaQAkHvE0KB-702M1Mhr/view?usp=drivesdk

๐Ÿ‘‰๐ŸฝK**a huwezi kupakua hii chati tafuta mtu akusaidie kuipakua na unaweza kwenda nayo stationery wakakuchapishia ukawa na nakala ngumu [hard copy]

๐Ÿ‘‰๐ŸฝChati hii ni ya sasso na tunaitumia kwa kuku chotara aina zote, hatuna chati za chotara wengine k**a unayo unaweza kuitumia.

2.Jambo la pili Jifunze kutumia hiyo chati kwa kuangalia hii video hapa kwa kubofya hii link ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ

https://youtu.be/ssrq3vHNL0o

๐Ÿ‘‰๐ŸฝK**a unapata changamoto kuangalia hii video tafuta mtu akusaidie namna ya kufungua hii video ya YouTube najua tunatofautiana!

3.Jambo la tatu hakikisha unawalisha kuku kwa kipimo kila siku k**a ambavyo hiyo chati inaonesha kiwango husika kwa kila siku

Hapa unahitaji mzani, k**a Bado huna mzani tupigie 0752 912132 kuagiza mzani wa kidijitali bei yake ni 20,000 na unapima kuanzia gram 100 mpaka kilo 50. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Moshi Agrovet tunapatikana Dodoma Majengo Sokoni

Zingatia kwamba kiwango cha chakula wanachokula kitakuwa kinabadilika kadri wanavyokua siku kwa siku

4.Ulishaji wa chakula ni asubuhi na mchana utagawa chakula nusu kwa nusu yaani k**a kuku wako chotara wanakula chakula kilo 20 kwa siku utawapa kilo 10 asubuhi na jioni utawapa kilo 10

๐€๐๐†๐€๐‹๐ˆ๐™๐Ž

Jifunze jinsi ya kuwalisha kuku wako kwa kufuata viwango vinavyoelekezwa kupitia hiyo chati

Tafadhali sisi hatutakufanyia hayo mahesabu ndio maana tumeandaa chati na hiyo video ili uweze kujifunza na kufanya wewe mwenyewe kila siku hapo bandani kwako.

Ni rahisi Wala sio ngumu

Asante sana kwa usikivu wako kwenye hili suala ๐Ÿ™๐Ÿฟ

CFP
Ulishaji wa uhakika

Kuku chotara 200 wenye umri wa siku 28 kwa siku watakula chakula kilo ngapi?Type jibu lako kwenye comment tujifunze pamo...
31/08/2026

Kuku chotara 200 wenye umri wa siku 28 kwa siku watakula chakula kilo ngapi?

Type jibu lako kwenye comment tujifunze pamoja ukiweka na maelezo itasaidia zaidi

Kuku chotara 150 kuanzia siku 1 mpaka siku 60 watakula chakula kilo ngapi?Andika jibu lako kwenye comment tujifunze pamo...
31/08/2026

Kuku chotara 150 kuanzia siku 1 mpaka siku 60 watakula chakula kilo ngapi?

Andika jibu lako kwenye comment tujifunze pamoja, ukiweka na maelezo itasaidia zaidi.

Hii chati tumeitoa pamoja na video ya namna ya kuitumia sijui k**a umeifuatilia ila majibu mengi yapo humu๐ŸŽฏFanya mambo h...
30/08/2026

Hii chati tumeitoa pamoja na video ya namna ya kuitumia sijui k**a umeifuatilia ila majibu mengi yapo humu๐ŸŽฏ

Fanya mambo haya Kujifunza zaidi...

1.Kwanza pakua hii chati ya kuku wa sasso ambayo utaitumia kujua kiwango cha chakula wanachokula kila siku kuanzia siku 1 mpaka siku 60

Kupakua hiyo chati bofya hii link hapa๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ

https://drive.google.com/file/d/1JyGNxKDUKYsQyaQAkHvE0KB-702M1Mhr/view?usp=drivesdk

๐Ÿ‘‰๐ŸฝK**a huwezi kupakua hii chati tafuta mtu akusaidie kuipakua na unaweza kwenda nayo stationery wakakuchapishia ukawa na nakala ngumu [hard copy]

๐Ÿ‘‰๐ŸฝChati hii ni ya sasso na tunaitumia kwa kuku chotara aina zote, hatuna chati za chotara wengine k**a unayo unaweza kuitumia.

2.Jambo la pili Jifunze kutumia hiyo chati kwa kuangalia hii video hapa kwa kubofya hii link ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ

https://youtu.be/ssrq3vHNL0o

๐Ÿ‘‰๐ŸฝK**a unapata changamoto kuangalia hii video tafuta mtu akusaidie namna ya kufungua hii video ya YouTube najua tunatofautiana!

3.Jambo la tatu hakikisha unawalisha kuku kwa kipimo kila siku k**a ambavyo hiyo chati inaonesha kiwango husika kwa kila siku

Hapa unahitaji mzani, k**a Bado huna mzani tupigie 0752 912132 kuagiza mzani wa kidijitali

Bei ya mzani ni 20,000 na unapima kuanzia gram 100 mpaka kilo 50. Pia unaweza kufika ofisini kwetu Moshi Agrovet tunapatikana Dodoma Majengo Sokoni

Zingatia kwamba kiwango cha chakula wanachokula kitakuwa kinabadilika kadri wanavyokua siku kwa siku

4.Ulishaji wa chakula ni asubuhi na mchana utagawa chakula nusu kwa nusu yaani k**a kuku wako chotara wanakula chakula kilo 20 kwa siku utawapa kilo 10 asubuhi na jioni utawapa kilo 10

5.Chati hii inaonesha uzito wa kuku kulingana na umri kwa kadri watakavyokua wanakua

๐€๐๐†๐€๐‹๐ˆ๐™๐Ž

Jifunze jinsi ya kuwalisha kuku wako kwa kufuata viwango vinavyoelekezwa kupitia hiyo chati

Tafadhali sisi hatutakufanyia hayo mahesabu ndio maana tumeandaa chati na hiyo video ili uweze kujifunza na kufanya wewe mwenyewe kila siku hapo bandani kwako.

Ni rahisi Wala sio ngumu

Asante sana kwa usikivu wako kwenye hili suala ๐Ÿ™๐Ÿฟ

CFP
Ulishaji wa uhakika

CFP ni virutubisho vinavyotumika kuandaa chakula cha kuku chotara kuanzia siku 1 mpaka unapowauza au wanapoanza kutaga U...
30/08/2026

CFP ni virutubisho vinavyotumika kuandaa chakula cha kuku chotara kuanzia siku 1 mpaka unapowauza au wanapoanza kutaga

Ukiwa na CFP unahitaji pumba za mahindi, mashudu ya alizeti, mahindi, mafuta na soya au dagaa kukamilisha chakula cha kuku wako.

Nikupe mfano wa chakula cha vifaranga kilo 100 kwa formula yenye mafuta ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ

Mahindi kilo 52
Soya kavu kilo 32
Mashudu ya alizeti kilo 9
Mafuta ya mboga kilo 2 [ Lita 2.26]
CFP ya vifaranga kilo 5

Jumla kilo 100

Ukitumia CFP huhitaji kuweka vitu vidogo k**a dcp, chokaa, premix,chumvi, Toxibinder kwasababu vitu hivyo vyote vipo ndani ya CFP

Rahisisha uchanganyaji wa chakula cha kuku wako kwa kutumia CFP

Tupigie 0752 912132 kuagiza CFP

Jinsi ya kuwalisha chotara siku 1-25๐Ÿ‘‰๐ŸฝKuku wa nyama tunahesabu umri wake katika siku, kuku wa mayai ndio wanaenda kwa wi...
30/08/2026

Jinsi ya kuwalisha chotara siku 1-25

๐Ÿ‘‰๐ŸฝKuku wa nyama tunahesabu umri wake katika siku, kuku wa mayai ndio wanaenda kwa wiki

๐Ÿ‘‰๐ŸฝUnapowapokea vifaranga wako utaanza kuwachanganyia starter mash watakula chakula hiki kuanzia Siku 1-25

๐Ÿ‘‰๐ŸฝKwa kawaida kuku mmoja anakula chakula kilo 1 kuanzia siku 1 mpaka siku 25

Hapa simaanishi kuwa kuku mmoja anakula chakula kilo 1 kila siku isipokuwa ukijumlisha chakula cha kuanzia siku 1 mpaka siku 25 jumla yake anakuwa amekula chakula kilo 1

Ili uweze kuelewa hili inabidi utofautishe kiwango cha Chakula anachokula kuku mmoja kwa siku (daily feed intake) na jumla ya kiwango cha Chakula anachokula kuku mmoja katika umri fulani (Cumulative feed intake)

Sasa tuchukulie mfano unataka kufuga chotara 500 je watakula chakula kilo ngapi kuanzia siku 1-25 ?

K**a kuku mmoja anakula kilo 1 siku 1 mpaka siku 25 maana yake kuku 500 watakula kilo 500

Kuku wako wakimaliza hii starter utaanza kuwachanganyia chakula cha grower

Mara chache inaweza kutokea wak**aliza chakula hicho mapema kidogo kabla ya siku 25, wanaweza kukimaliza siku 22 au 23

Ikitokea hivyo utaanza kuwachanganyia chakula cha grower kuanzia siku 22 au 23 walipomaliza chakula

Muhimu : Hakikisha umewapa starter kwa kiwango kinachotakiwa kabla ya kuanza kuwapa grower

Formula ya cha chakula vifaranga nikupe mfano wa kilo 100

Mahindi paraza kilo 52
Soya kavu kilo 32
Mashudu ya alizeti kilo 9
Mafuta/oil kilo 2
CFP ya vifaranga kilo 5

Jumla kilo 100, itakupa matokeo mazuri na utasevu sana hela
Mafuta unaweza kutumia alizeti, korie, safietc

K**a unahitaji CFP ya vifaranga tupigie 0752912132 tunapatikana Dodoma, Majengo Sokoni

Idadi ya kuku na kilo zinazohitajika siku 1-25 kulingana na idadi ya kuku

๐Ÿ‘‰๐ŸฝKuku 100 watakula chakula cha starter kilo 100

๐Ÿ‘‰๐ŸฝKuku 200 watakula chakula cha starter kilo 200

๐Ÿ‘‰๐ŸฝKuku 300 watakula chakula cha starter kilo 300

๐Ÿ‘‰๐ŸฝKuku 400 watakula chakula cha starter kilo 400

๐Ÿ‘‰๐ŸฝKuku 500 watakula chakula cha starter kilo 500

Address

Fatina/Majengo Soko Kuu Karibu Na CRDB
Dodoma

Opening Hours

Monday 07:00 - 19:00
Tuesday 07:00 - 19:00
Wednesday 07:00 - 19:00
Thursday 07:00 - 19:00
Friday 07:00 - 19:00
Saturday 07:00 - 19:00
Sunday 09:00 - 16:00

Telephone

+255659632332

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Moshi Agrovet posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Restaurant

Send a message to Moshi Agrovet:

Shortcuts

Share