BEHAC Company Limited

BEHAC Company Limited we are business company based in Dar es salaam. Offering a variety of services.

01/01/2026

Heri ya Mwaka Mpya 2026
Mwaka jana 2025 nilisema nitaongelea *Kwa nini tufanye Biashara Moja tu hata k**a tuna uwezo wa kuanzisha zaidi ya moja?*
Hizi hapa ndio sababu zenyewe:-
Kumbuka kwenye somo la kwanza la mwaka jana 2025 tuliangazia ni Biashara ipi unapaswa ufanye na tukasema ni ile unayoipenda na kuijua vizuri.
Kwa kuzingatia hilo leo ni mwendelezo kwenye hili somo la pili.
Sababu ya kwanza ya kuepuka kuwa na Biashara zaidi ya moja:
1.Kuwa na muda wa kutosha kuisimamia biashara hiyo.
Maana biashara unapoianzisha inahitaji mwanzilishi awe karibu sana k**a mtoto mdogo anavokuwa karibu na mama yake pindi anapozaliwa, kadiri unavyozidi kukua ndio uboreshaji wa mifumo ya uendeshaji huhitajika.
Ukianzisha zaidi ya moja ni dhahiri umejipanga kufeli au kuchelewa kukua kwenye Biashara.
Kuwa na Biashara zaidi ya moja hii ni hatua ya pili baada ya hatua hii ya kwanza *kufanikiwa.*
Biashara kufanikiwa ni nini?
Biashara inakuwa haikuhitaji wewe uwepo ndio itoe huduma, haihitaji hela za mfukoni kwako ndio iende.
Hapo ndipo Biashara zingine za ya moja huzaliwa maana utakuwa unaanzisha kwa lengo la kusapoti huduma au biashara mama na hapo hapo nayo inakuwa inaingiza pesa.
Mfano:Una biashara ya mazao, biashara ikafanikiwa ukaamua ununue Lori ili iwe rahisi kuwahudumia wateja wako,hapo hapo utapanga mfumo wa kuhudumia wengine na kuanza kupata hela nyingine.
Ongezea zingine
2.
3.
Kwa upande wangu kabla sijaanza kufanya biashara nilisoma vitabu mbalimbali na kukutana na wengi kwenye biashara na wote ili kuwa ni kuanzisha biashara moja na si zaidi ila niliona wananitania,nikaona wananichelewesha kuwa na hela, maana hela ninayo ya kuanzisha biashara zaidi ya moja kwa nini nisifanye?
Niliamua kuiacha kanuni na kutengeneza kanuni yangu ya kuvuna mihela mingi na jibu hela nilizizika na kubakiwa na biashara moja.
Saivi nafata masharti naendelea vizuri,sasa na wewe mpendwa wa Mungu usije ukakaidi ukapata hasara.
*Somo la tatu litakuwa kwa nini hupaswi kuanza na mtaji mkubwa sana na ba

31/12/2025

Ndugu Wateja wangu
Naomba ni share nanyi leo
UZOEFU WANGU KWENYE
*BIASHARA*
1.Fanya biashara unayoipenda na kuijua vizuri.

*Unayoipenda*
Kitu kipo moyoni
Mfano: Unapenda kuongea kiingereza kila mara
Unapenda kusaidia watu
Unapenda kufundisha watu

*Kuijua vizuri*
Una uelewa wa jambo hilo.
Mfano:Unajua kutengeneza pikipiki ikiharibika bila shaka
Unajua kufundisha somo la Hisabati bila kufoji kanuni wala taratibu za kimahesabu.

*Kuipenda+Kuijua vizuri=Biashara unayotakiwa kufanya.*

Usipotumia kanuni hii mwakani *2026* pia usitegemee kukua kwenye Biashara yako.
Nasema haya kwa sababu nilifanya Biashara hizi kwa kuzipenda tu na *zilikufa*
1.Kufuga kuku 2019 tukiwa na rafiki yangu Justine Faustine Stephano Old Shinyanga tuliweka milioni 3 zikapotea.
2.Biashara ya uwakala mpesa,Halopesa, Airtel money Shinyanga mjini Bwalo la polisi 2021 niliweka milioni 26 zikafa.
3.Bar milioni 5 zikafa.
4.Mgahawa ulijulikana BEHAC Food court Shinyanga mjini ukafa.

Hizo ni baadhi tu, lengo ni nini?
1.Nilizipenda sana kulingana na namna nilivoona waliokuwa wanazifanya walipa hela na Mafanikio mengi makubwa.
Leo naomba usipende biashara kwenye moyo wako na kuifanya bila hata kuijua vizuri.

Ukipenda kuuza vifaa vya ujenzi basi unatakiwa uwe unajua hata kujenga vizuri ili mteja akija ana kiasi kidogo na anataka kujenga nyumba nzuri umshauri kitaalamu sio kumpa buraburaa tu.
Kuanzia leo nitajitahidi kubadilishana uzoefu wangu na wewe ili ujenge biashara imara na endelevu.
Je biashara inayoifanya ikitokea mfanyakazi au wafanyakazi wako wakagoma kuja kazini utatoa huduma kikamilifu?
Dondosha comments.

https://youtube.com/-j1u?si=Vpvb5R9dGyMYg8-5
09/08/2025

https://youtube.com/-j1u?si=Vpvb5R9dGyMYg8-5

We encourage kids of anywhere to learn. For more informations: 0738~707977~Call/sms 0625~413694~Call/sms 0782~768524~WhatsApp Facebook~BEHAC company limited Instagram ~behaccompany Tiktok~kids.learning.platform. Youtube~Kids Learning Platform You are Welcome.

Mlete mwanao tunamsubiri.
01/08/2025

Mlete mwanao tunamsubiri.

We call you to support us by bringing your kid to our lovely school. Subscribe to our channel.

29/07/2025

Letter Sounds revisions.

Usisahau ku subscribe kwenye channel yetu.
29/07/2025

Usisahau ku subscribe kwenye channel yetu.

Letter Sounds revisions.

Usisahau ku subscribe ili uwe sehemu ya madarasa yetu.
29/07/2025

Usisahau ku subscribe ili uwe sehemu ya madarasa yetu.

Omit and Replace the first letter sound to form new word.

Address

Po Box 45563
Dar Es Salaam
00000

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when BEHAC Company Limited posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share