20/09/2026
KILE ALICHOSEMA ZEKARIA
Ndugu na Dada Katika Mwili wa Kristo, kwa Unyenyekevu Mkubwa, Karibu tujifunze pamoja kile Zekaria alichomaanisha aliposema haya yafuatayo;
[16] Hata itakuwa, ya kwamba kila mtu aliyesalia wa mataifa yote, waliokuja kupigana na Jerusalem, atakwea mwaka baada ya mwaka ili "Kumwabudu Mfalme", ADONAY wa majeshi, na kuishika Sikukuu ya "Vibanda".
Katika hili, Kuna mambo matatu yanayopelekea "Sikukuu ya Vibanda" kuwa Maalumu mbele za Mungu, na mbele za watu wake ISRAEL, na Kanisa la Kristo.
â™§ UNYENYEKEVU: K**a vile wana wa ISRAEL walivyokaa Vibanda Jangwani kwa miaka 40, vivyo hivyo, hata leo Mungu anataka watu wake tuendelea Kukumbuka.
(Lawi:23:42,43)
[42] Mtakaa katika "Vibanda" muda wa siku 7 ; wazalia wote wa ISRAEL watakaa "vibadani";
[43] ili vizazi vyenu vipate kujua ya kuwa "Niliwaketisha wana wa ISRAEL katika vibanda, hapo "Nilipowaleta" kutoka nchi ya Misri: Mimi ndimi "ADONAY ELOHEINU" wenu.
B) KUMTEGEMEA: Wana wa ISRAEL, walimtegemea Mungu kwa kila jambo muda wa miaka 40 Jangwani, Naye 'akawatimizia' haja zao zote.
(Kumbukumbu la Torati 8:2)
[2] Nawe utaikumbuka njia ile yote ADONAY, ELOHEINU wako aliyokuongoza miaka hii 'arobaini' katika jangwa, ili 'akutweze' 'kukujaribu' kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo.
C) MAVUNO: Mwisho wa Ulimwengu, watu wote watavunwa na kurejea kwa Muumba wao; waliotenda Mema kwa ajili ya "Uzima wa milele", waliotenda Mabaya kwa ajili ya Hukumu ya milele na milele.
(Mathayo 13:39)
[39] Yule adui ni Ibilisi; Mavuno ni mwisho wa Dunia; na wake wavunao ni Malaika.
(Yoel 3:13)
[13]Haya! Utieni 'mundu', maana "mavuno yaneiva"; Njoni, kanyageni; kwa maana shinikizo limejaa, mapipa nayo yamefurika; kwani uovu wao ni mwingi sana.
Ndugu na Dada Katika Mwili wa Kristo, huu ndio Kweli ya {"Sukkoth au Vibanda"} si kwa ajili ya ISRAEL peke yao, hata sisi Kanisa la Kristo inatuhusu.
"Sukkoth au Vibanda"
Je! "Sukkoth au Vibanda" leo Ni nini hasa? Sikukuu ya Vibanda, au Sukkoth ni "Kumbukizi" ya Namna wana wa ISRAEL, walivyoishi ndani ya Vibanda muda wa miaka 40.
Mungu Mwenyewe Ndiye aliyesema k**a tulivyoona pale juu, Unauliza, na Sisi Kanisa kwa maana ya mwili wa Kristo Sukkoth au Vibanda inatuhisu?
▪︎ Naam, Sukkoth au Vibanda inatuhusu wote, kwa vile, wana ISRAEL wanapokumbuka walivyoishi katika Vibanda, Sisi tunakumbuka tulivyoishia Katika Dhambi mbali na Mungu.
▪︎ Lakini pia, inatupa nafasi ya Kutafakari Ukuu na Uweza wake wa Wokovu, na Namna ile Alivyotuokoa toka dhambini.
Bila shaka, Umeona vile ilivyomhimu, Jiandae Kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda mwaka 2027 ujao.
Ni Katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareth, naweka katika Uwezo wa Mungu ili Ulindwe Salama. Amina na Amina tena Amina.