01/08/2026
Uhalifu Nanyuki.
Mnamo tarehe 31 Julai 2026 saa 1:34 jioni, kijana mmoja anaingia katika duka moja katikati ya mji wa Nanyuki linalouza simu na vifaa vya kielektroniki. Anaonekana kuwa na ujasiri wa mtu ambaye huenda amewahi kufanya jambo k**a hili hapo awali au alikuwa amelifanyia upelelezi duka hilo mapema.
Anaweka blaza yake kwenye rafu na kuomba kuonyeshwa nyaya za umeme (extension cables) zinazouzwa.
Muuzaji analazimika kuinama kuzitoa kwenye rafu. Wakati huo anaacha simu yake juu ya kaunta. Kijana huyo anajaribu kuichukua, lakini muuzaji anainuka haraka kabla hajafanikiwa.
Anaomba kuonyeshwa aina nyingine za extension cables. Wakati huo anaendelea kuchezea kitabu na nyaya hizo, akiziweka juu ya simu ili kuficha alichokuwa akikusudia.
Mhalifu mwenzake tayari yupo ndani ya duka, upande mwingine. Naye anaonekana kuvutiwa na bidhaa fulani, lakini lengo linaonekana kuwa ni kumtoa muuzaji kwenye kaunta na kumvuruga mawazo.
Ndipo kijana huyo mhalifu anavaa blaza yake, anaingiza simu mfukoni kwa siri na kuondoka kwenye kaunta. Anapopita karibu na muuzaji na mwenzake, anaweka extension cable pembeni yao na kusema anaenda kutafuta chenji.
Huo ndio ulikuwa mwisho wa kuonekana kwake.
Muda mfupi baadaye, mwenzake naye anaondoka.
Kulikuwa na dalili ambazo baadaye zinaonekana wazi, lakini tusimlaumu muuzaji. Hakuna anayepaswa kulaumiwa kwa kuwa mwathirika wa uhalifu. Unless uko upande wa wezi, hupaswi kulaumu mhudumu.
Namna ambavyo wakora hawa wawili walitekeleza tukio hili inaonyesha huenda walikuwa wamejipanga na kulizoea. Wasipok**atwa, kuna uwezekano wakawalenga wafanyabiashara wengine.
Tukio hili limeripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Nanyuki, na tunatoa wito kwa polisi kufanya uchunguzi wa haraka na kuwachukulia hatua wahusika.
Jana walitumia extension cables k**a kisingizio. Leo inaweza kuwa duka la dawa. Kesho inaweza kuwa sehemu ya burudani. Baadaye wanaweza kulenga uhalifu mkubwa zaidi.
Huu ni ujumbe wa tahadhari kwa wafanyabiashara wote katika eneo hili. Kuwa macho. Kuna wahalifu wanaozunguka.
Iwapo unawatambua wezi hawa wawili kupitia picha za CCTV, tafadhali toa taarifa ili sheria ichukue mkondo wake.